Exodus 25:8-40

8 a“Kisha uwaamuru wanitengenezee mahali patakatifu, nami nitakaa miongoni mwao. 9 bTengeneza hema hili na vyombo vyake vyote sawasawa na kielelezo nitakachokuonyesha.

Sanduku La Agano

(Kutoka 37:1-9)

10 c“Nao watatengeneza Sanduku la mbao za mshita, lenye urefu wa dhiraa mbili na nusu,
Dhiraa mbili na nusu ni sawa na sentimita 112.5.
upana wa dhiraa moja na nusu,
Dhiraa moja na nusu ni sawa na sentimita 67.5.
na kimo cha dhiraa moja na nusu.
11 fUtalifunika hilo Sanduku kwa dhahabu safi ndani na nje, na kulifanyia ukingo wa dhahabu juu yake kulizunguka. 12Utalisubu kwa pete nne za dhahabu na kuzifungia kwenye miguu yake minne, pete mbili kwa upande mmoja na pete mbili kwa upande mwingine. 13 gKisha utatengeneza mipiko ya mti wa mshita na kuzifunika kwa dhahabu. 14 hUtaiingiza hiyo mipiko kwenye zile pete katika pande mbili za Sanduku ili kulibeba. 15 iHiyo mipiko itabakia daima katika hizo pete za hilo Sanduku; haitaondolewa. 16 jKisha weka ndani ya hilo Sanduku ule Ushuhuda nitakaokupa.

17 k“Tengeneza kifuniko cha upatanisho cha dhahabu safi, chenye urefu wa dhiraa mbili na nusu, na upana wa dhiraa moja na nusu. 18 lTengeneza makerubi wawili wa dhahabu iliyofuliwa katika miisho ya hicho kifuniko. 19Tengeneza kerubi mmoja kwenye mwisho mmoja, na kerubi mwingine kwenye mwisho mwingine; watengeneze makerubi hao wawe kitu kimoja na hicho kifuniko katika miisho hiyo miwili. 20 mMakerubi hao watakuwa wametandaza mabawa kuelekea juu, yakitia kivuli hicho kifuniko. Makerubi hao wataelekeana, wakitazama hicho kifuniko. 21 nWeka huo Ushuhuda nitakaokupa ndani ya hilo Sanduku la Agano, na uweke hicho kifuniko juu ya hilo Sanduku. 22 oHapo juu ya hicho kifuniko, kati ya hao makerubi wawili walioko juu ya hilo Sanduku la Ushuhuda, hapo ndipo nitakapokutana nawe na kukupa maagizo yangu kwa ajili ya Waisraeli.

Meza Ya Mikate Ya Wonyesho

(Kutoka 37:10-16)

23 p“Tengeneza meza ya mbao za mshita yenye urefu wa dhiraa mbili,
Dhiraa mbili ni sawa na sentimita 90.
upana wa dhiraa moja, na kimo cha dhiraa moja na nusu.
24Ifunike kwa dhahabu safi, na kuitengenezea ukingo wa dhahabu kuizunguka pande zote. 25Kisha tengeneza upapi wenye upana wa nyanda nne,
Nyanda nne ni sawa na sentimita 8.
na ufanyie ule upapi ukingo wa dhahabu kuuzunguka pande zote.
26Tengeneza pete nne za dhahabu kwa ajili ya meza hiyo, na uzifungie kwenye pembe nne, pale penye miguu yake minne. 27Pete hizo zitakuwa karibu na ukingo ule ili kuishikilia ile mipiko itakayotumika kuibebea hiyo meza. 28Tengeneza mipiko hiyo kwa mbao za mshita, uifunike na dhahabu, uitumie kubeba hiyo meza. 29 sTengeneza sahani zake na masinia yake kwa dhahabu safi, pamoja na bilauri na bakuli zake kwa ajili ya kumiminia sadaka. 30 tUtaweka mikate ya Wonyesho juu ya meza hii iwe mbele yangu daima.

Kinara Cha Taa

(Kutoka 37:17-24)

31 u“Tengeneza kinara cha taa cha dhahabu safi iliyofuliwa vizuri katika kitako chake na ufito wake; vikombe vyake vinavyofanana na ua, matovu yake na maua yake viwe kitu kimoja. 32 vMatawi sita yatatokeza kuanzia ule ufito wa katikati wa kinara cha taa: matawi matatu upande mmoja na matatu upande mwingine. 33Vikombe vitatu vya mfano wa maua ya mlozi yenye matovu na maua vitakuwa katika tawi moja, vikombe vitatu katika tawi jingine, na vivyo hivyo kwa matawi yote sita yanayotokeza kwenye kile kinara cha taa. 34Juu ya kinara chenyewe vitakuwepo vikombe vinne vya mfano wa maua ya mlozi yakiwa na matovu yake na maua yake. 35Tovu moja litakuwa chini ya jozi ya kwanza ya matawi yaliyotokeza kwenye kinara cha taa, tovu la pili chini ya jozi ya pili, nalo tovu la tatu chini ya jozi ya tatu, yaani matawi sita kwa jumla. 36 wMatovu na matawi yote yatakuwa kitu kimoja na kile kinara cha taa, yakifuliwa kwa dhahabu safi.

37 x“Kisha tengeneza taa zake saba na uziweke juu ya kinara hicho ili ziangaze mbele yake. 38 yMikasi ya kusawazishia tambi, pamoja na masinia, zote zitakuwa za dhahabu safi. 39Utatumia talanta moja
Talanta moja ya dhahabu ni sawa na kilo 34.
ya dhahabu safi kutengeneza hicho kinara na vifaa vyake vyote.
40 aaHakikisha kuwa umevitengeneza sawasawa na ule mfano ulioonyeshwa kule mlimani.

Copyright information for SwhNEN